Hujambo mkereketwa wa Kiswahili. Karibu katika wavuti huu wa Kiswahili Mujarabu. Ninashukuru kwa kupata fursa na satua hii kuweka pamoja sahifa za tovuti hii ili kuelekeza machache yaliyopo katika uwanja mpana wa Kiswahili kinachofundishwa katika shule za msingi nchini Kenya.
Yaliyomo ni pamwe na:
- Misamiati mbalimbali
- Kusoma
- Kusikiliza na kuongea
- Uandishi aula wa Insha
- Sarufi
- Mawasia tofauti tofauti ya ufundishali wa vipengele vya lugha.
- Maswali mseto ya vipengele tofauti tofauti
Mambo yaliyopo katika wavuti huu ni yale yaliyotokana na mkusanyiko wa kazi na tajriba ya zaidi ya mwongo u nusu. Litakuwa jambo la busara tukiungana pamoja nawe kukikuze na kukipe hadhi Kiswahili huku nchini Kenya na ughaibuni.
Una huria kuniandikia maoni au barua pepe katika anwani iliyoko katika pembezo ya chini katika ukurasa huu. Ninashukuru kwa muda wako wa kusoma na kuungana nami katika jambo hili kabambe.
Wako wa dhati,
Mdarisi Bundi Mbijiwe
Kiswahili Mujarabu