Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Month: June 2021

Taswira Jozi

Posted on By 6 Comments on Taswira Jozi

Haya ni maneno yaliyo na maana moja na huumika katika jozi ili kuleta msisistizo katika uzungumzaji au uandishi. Sana sana huwa vitenzi. Tazama mifano ifuatayo:

1. Ardhi na mbingu – tofautiana

2. Asili na jadi -zamani sana.

3. Balaa na belua – matatizo makubwa.

4. Bure bilashi – bila sababu yoyote ile.

5. Daima dawamu – bila kukoma; kila wakati.

6. Doto na Kurwa – pacha

Tafadhali Soma Zaidi “Taswira Jozi” »

Kusikiliza na kuongea

Majina ya Makundi

Posted on By 6 Comments on Majina ya Makundi

1. Almashauri ya shule

2. Biwi la takataka / simanzi

3. Bunda la noti / kititacha pesa

4. Chane ya ndizi

5. Doti ya kanga

Tafadhali Soma Zaidi “Majina ya Makundi” »

Kusikiliza na kuongea

Tashbihi au Tashbiha

Posted on By 6 Comments on Tashbihi au Tashbiha

Tashibihi ni maneno ya mfananisho wa wazo na jingine kwa kutumia maneno kama, sawasawa na, mfanano na, mithili ya, ungedhani nk. Tazama mifano ifuatayo:

 1. Adimika kama wali wa daku; barafu ya kukaanga; kaburi la baniani; kivuli cha nzi; maziwa ya kuku.

2. Amrisha kama mwanajeshi.

3. Angalia huku na huko kama luja.

4. Angua kicheko kama radi, jitu, fisi.

5. Bahati kama mtende; mwana aliyezaliwa Ijumaa.

Tafadhali Soma Zaidi “Tashbihi au Tashbiha” »

Kusikiliza na kuongea

Visawe

Posted on By 6 Comments on Visawe

Visawe aidha sinonimia ni maneno ambayo maana yake inakaribiana sana. Ukipenda ni maneno yaliyo na maana moja.
Tazama mifano ifuatayo:
1. Afya – siha.
2. Aibika – susuwaa, fedheheka, tahayari.
3. Ajabu – shani, kioja, kituko, muujiza, dungudungu, hekaya.
4. Angamiza – hilikisha, tilifisha.
5. Asali – uki.

Tafadhali Soma Zaidi “Visawe” »

Kusikiliza na kuongea

Shadda au Takriri

Posted on By 6 Comments on Shadda au Takriri

1. Asili na jadi – zamani za kale 2. Balaa na beluwa – matatizo makubwa. 3. Bure bilashi – bila sababu yoyote – bila sababu yoyote. 4. Daima dawamu – kila wakati/ bila kukoma. 5. Dhahiri shahiri – jambo lililo wazi 6. Enzi na dahari – tangu zamani. 7. Hali na mali – kwa kila…

Tafadhali Soma Zaidi “Shadda au Takriri” »

Kusikiliza na kuongea

Wasifu

Posted on By 6 Comments on Wasifu

Insha ya wasifu kama lilivyo jina lake ni mtungo unaosifu kitu, mahali, mtu au nchi. Sifa zinazotolewa huwa zimewanda na hutokana na mada husika. Kila mada hushulikiwa kivyake japo yapo mambo yanayoangaziwa katika kila mada. Mwanafunzi ashughulikie yafuatayo: a)    Jina la kitu, mtu, mahali, nchi na kadhalika. b)    Uhusuhano wa jamaa au jamii ya vitu….

Tafadhali Soma Zaidi “Wasifu” »

Aina za insha

Mdokezo

Posted on By 6 Comments on Mdokezo

Dondoo au mdokezo ni insha ambayo mtahiniwa hupewa mwanzo au mwisho wa hadithi. Mtahiniwa huhitajika kutoa kisa kinachodhihrisha na kulenda maudhui yanayoafikiana na mdokezo ule aliopewa. Mwanafunzi anahitajika kuwa na utangulizi ulio na mvuto. Mwili wa insha ulenge maudhui kwa kina. Ahitimishe kwa wazo la kukumbukwa au wasia mwafaka. Mwanafunzi anahija kuangazia mambo kadhaa ili alenge maudhi…

Tafadhali Soma Zaidi “Mdokezo” »

Aina za insha

Usahihishaji wa insha ya masimulizi katika mitihani ya taifa (K.C.P.E)

Posted on By 6 Comments on Usahihishaji wa insha ya masimulizi katika mitihani ya taifa (K.C.P.E)

01 – 06 (daraja A) Maudhui huenda yasipatikane au yakiwapo yawe hafifu sana. Pengine hujirudiarudia. Msamiati umetumika holelaholela bila kuzingatia usawa wowote. Pengine yatokee maneno yasiyo ya Kiswahili. Mtindo na muundo haujaumbika. Mtahiniwa anajaribu kusimulia. Aya zipo hata kama yaliyomo hayatambuliki. Hati inasomeka. Mshikamano na Mtiririko huenda usiwapo kwa ukosefu au huafifu wa mawasiliano. 07…

Tafadhali Soma Zaidi “Usahihishaji wa insha ya masimulizi katika mitihani ya taifa (K.C.P.E)” »

Utahini wa Insha KCPE

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme