Hizi ni ngeli maelezo yake na maneno kadhaa yanayopatikana katika kila ngeli.
NGELI | MAELEZO | Mifano |
A – WA | Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai, vinavyoonekana na visivyoonekana. Majina ya ngeli hii hayana mianzo maalum. | Mtu – Watu
Malaika – Malaika Mwalimu – Walimu Daktari – Madaktari Nyani – Manyani Bata – Mabata |
KI – VI | Hii ni ngeli ya majina ya vitu hasa visivyo na uhai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Aidha majina yote yaliyodunishwa huwekwa katika ngeli hii. | Cherehani – Vyerehani
Kitoto – Vitoto Kiatu – Viatu Choo – Vyoo Kisu – Visu Chano – Vyano |
LI – YA | Ngeli hii hujumuisha majina ya vitu visivyo hai pamoja na yale ya hali ya ukubwa. Maneno haya huchukua MA- katika hali ya wingi. | Jani – Majani
Goti – Magoti Dirisha – Madirisha Toto – Matoto Fupa – Mafupa Vumbi – Mavumbi |
U – I | Ngeli hii huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M, MW na MU- (umoja) na MI(wingi). | Mti – Miti
Mtulinga – Mitulinga Mwili – Miili Muwa – Miwa Mwezi – Miezi |
U – ZI | Ngeli hii hurejelea majina mengi ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina haya huchukua ny, ng, mb, nd na nj katika wingi. Mengine hupoteza mwanzo U. | Ukuta – Kuta
Ubavu – Mbavu Wembe – Nyembe Uzi – Nyuzi Ugavu – Ngavu Udevu – Ndevu |
I – ZI | Ngeli hii hujumlisha majina ya kawaida yasiyobadilika katika umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). Hayana mianzo maalum. | Nyumba – Nyumba
Hospitali – Hospitali Katarasi – Karatasi Sufuria – Sufuria Sakafu – Sakafu |
U – YA | Ngeli hii huwa ya majina mengi yaliyo na mianzo ya U katika umoja na YA katika wingi. | Uwele – Mawele
Ulezi – Malezi Ugonjwa – Magonjwa Uuaji – Mauaji Ubua – Mabua |
YA – YA | Ngeli hii ni ya vitu visivyohesabika. Majina haya hayana umoja. Mengi ya majina haya huanza kwa Ma-. | Maji – Maji
Mafuta – Mafuta Maziwa – Maziwa Marashi – Marashi Mazingira – Mazingira Mali – Mali |
KU – KU | Hii ni ngeli ya vitenzi-majina. Maneno yote ya vitenzi hupachikwa KU mwanzoni yakawa vitenzi-majina. Maneno haya hayana wingi. | Kuiba – Kuiba
Kuruka – Kuruka Kusoma – Kusoma Kupenda – Kupenda Kulala – Kulala Kupika – Kupika |
I-I | Ngeli hii ni ya majina ya wingi. Majina mengi huwa na mianzo ya mi-. | Sukari – Sukari
Mvua – Mvua Miraa – Miraa Mikogo – Mikogo Mizani – Mizani Miradhi – Miradhi |
U – U | Majina ya nomino za wingi yanayoanza kwa mianzo ya u- Hayana wingi. Vile vile sifa za vitu, vuimbe na matendo huwekwa hapa. | Unga – Unga
Ugali – Ugali Uyoga – Uyoga Ulevi – Ulevi Uhodari – Uhodari Uzuri – Uzuri |
PA – PA | Hii ni ngeli ya mahali mahali pa juu panapodhihirika, panapogusika. | Mezani Pale.
Uwanjani Hapo. Kiatuni Hapa. |
KU – KU | Ngeli hii ni ya mahali kwa ujumla. | Uwanjani Huku.
Sokoni Huko. Shambani Kule. |
MU – MU | Ngeli hii ni ya mahali mwa ndani. | Shimoni Humu.
Darasani Humo. Shimoni Mle. |