Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Insha ya Methali

Posted on By Harun Mbijiwe 6 Comments on Insha ya Methali

Insha ya Methali baadhi ya uandishi unaohitaji ufundi na kusukwa kwa umakinifu. Kwanza lazima mwanafunzi aeleze maana ya nje na ndani ya methali. Ajue kuwa methali huwa na sehemu mbili; hivyo ni kusema swali na jibu au tatizo na suluhisho. Kwa mfano; Asiye na wake (swali) ana Mungu (jibu).

Atoe methali nyingine yenye maana sawa na hiyo. Baada ya hili, aandike kisa au mkasa wa kusisimua unaoambatana na Methali yenyewe. Itakuwa vizuri sana akimalizia kwa wazo kuu na methali iliyo na maana sawa na hiyo.

Tanibihi:

a)    Mwanafunzi ashughulikie na ateue wahusika vizuri.

b)  Anapotoa kisa au mkasa ashughulikie hadithi katika wakati wake. Asichanganye nyakati kwa mfano zipo hadithi mambo sasa na mambo zamani. Kama kisa chake kitakuwa na mwanzo wa, ‘Hapo zamani za kale…’ basi adumu katika zamani hizo asichanganye na mambo leo kama vile UKIMWI, magari, masomo n.k.

c)  Iwapo hajui maana ya methali na yuajua kisa kinachoweza kulandana na wazo kuu la methali, atoe kisa moja kwa moja pasi kuandika maana ya methali. Ni vyema kufanya hivyo badala ya kutoa maana asiyoijua ipotoshe insha zaidi.

d)  Aandike kisa kilicho na maadili na lugha tasfida.

Post Views: 196
Aina za insha Tags:Insha ya Methali

Post navigation

Previous Post: Tashbihi
Next Post: Barua

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme