Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Barua

Posted on By Harun Mbijiwe 6 Comments on Barua

BARUA

Barua ni mtungo unaowasilisha ujumbe kwa mtu mwengine labda kwa kutumwa kwa njia ya posta au mtu mwengine (tarishi).

Zipo aina mbili za insha za barua. Barua ya kirafiki na barua rasmi.

BARUA RASMI:

Huandikwa kwa sababu ya sababu fulani maalum. Inaweza kuandikwa kwa kuomba nafasi ya kazi, kuomba msamaha kazini, kuomba uhamisho, kuomba nafasi katika shule na kadhalika. Hushughulikia mambo rasmi na muhimu pekee.

Mtindo na muundo wake sharti ufuatilie vipengele vifuatavyo.

  1. Sharti iwe na anwani mbili. Moja katika upende wa kulia ya mwandishi na nyingine ya mwandikiwa. Tarehe huandikwa pamoja na anwani ya mwandishi.
  2. Pawe na salamu au kianzio.
  3. Pawe na mtajo ambao hupeana makusudio ya uandishi ambao una vianzio tofaututofauti kama vile:
    1. YAH: Yahusu
    2. KUH: Kuhusu
    3. KU: Kuhusu
    4. MINT: Mintarafu
  4. Katika mwili, maelezo bayana au shabaha kamili huelezewa kwa kina.
  5. Hitimisho, wasaalam au kimalizio huandikwa wako mwaminifu au wako mtiifu. Katika sehemu mtahiniwa atie sahihi na aandike jina lake kamili. Angalia mfano katika sehemu ya INSHA SHESHE ukurasa _______.

BARUA YA KIRAFIKI

Barua hii hususan huandikiwa ndugu awaye yule. Anaweza kuwa wa aila ya mwandishi au rafiki yeyote yule. Hutumika katika kujuliana hali au kuelezea matukio katika mandhari waliomo.

Barua hii huwa na anwani ya mwandishi upande wa kulia, tarehe vile vile chini ya anwani hiyo.

Baada ya anwani pawe na mtajo kuelekeza inaendea nani yaani mwandikiwa.

Baada ya hayo utangulizi hushughulikia salamu kwa mwandikiwa au kumjulia hali.

Aya ya pili huwa ni mtajo wa madhumuni au nia ya kuandika barua yenyewe. Vile vile mwandishi huanza kushughulikia maudhui kutoka sehemu hii kuendelea.

Hitimisho huwa ni wazo kuu kwa mwandikiwa pamoja na kumwomba mwandikiwa kuwapa wengine salamu za mwandishi.

Baada ya kukamilisha sehemu ya mwili wa insha, Mwanafunzi humalizia kwa kimalizio cha wako mpendwa, rafiki, dada, kaka, wa roho n.k. mwandishi huandika jina lake kamili.

Post Views: 160
Aina za insha Tags:insha ya barua

Post navigation

Previous Post: Insha ya Methali

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme