Kielezi ni neno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi, kivumishi au kielezi.
a) Vielezi wakati (Adverbs of time)
Tutaonana mwakani.
Mzee mlevi alifika usiku wa manane.
b) Vielezi mahali (Adverbs of place)
Wameondoka kwenda cheteni.
Ndege wameingia kiotani.
c) Vielezi jinsi au namna (Adverbs of manner)
Amecheza kwa ustadi.
Walimaliza chakula haraka.
d) Vielezi kiigizi (Adverbs of interjection)
Alianguka mchangani tifu!
Njia imenyoka twa!
e) Vielezi mkazo
Tumeelezwa mambo yote dhahiri shahiri.
Mama alimchapa mwanawe bure bilashi.
f) Vielezi namna vikariri/takriri
Alibebwa hobelahobela.
Anatembea asteaste.
g) Vielezi idadi au kiasi (Adverb of degree)
Aghalabu tutakuwa tukionana.
Amekula matunda mengi.
h) Vielezi tashibihi
Alijuta kama Filauni.
Walivumilia mateso kama watumwa.
i) Vielezi kiulizi (interrogative adverb)
Mtaniletea nini?
Ameondoka kwenda wapi?