Abjadi ni nini?
Abjadi au alfabeti ni sauti 30 za lugha ya Kiswahili. Hata hivyo tukirejelea kamusi kuu ya TUKI tutapata 31. Herufi C, Q na X hazipo katika alfabeti. Tazama herufi sifuatazo:-
- a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ng’, ny, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z.
- Herufi Kh imeongezewa katika kamusi ya tuki.
Tunaweza kugawanya herufi hizi mara mbili.
Voweli au irabu (5)
a, e, i, o, u
Konsonanti (25)
b, ch, d, dh, f, g, gh, h, j, k, kh, l, m, n, ng’, ny, p, r, s, sh, t, th, v, w, y, z.
Silabi
Silabi huundwa kwa kutumia herufi ya konsonanti na voweli moja. Hutamkwa kama sauti moja. Kwa mfano:
- ch + a = cha
- m + e = me
- z + i = zi
- dh + o = dho
kwa hivyo:
Neno hobelahobela lina silabi 6 – ho + be + la + ho + be + la
Neno mwanafunzi lina silabi 4 – mwa + na + fu + nzi
Sauti
Sauti za Kiswahili ni abjadi au alfabeti ya Kiswahili. Neno lolote la Kiswahili huundwa kwa sauti hizi. Zinaweza kuwa konsonanti au voweli.
Mifano katika maneno:
Neno kiatu lina sauti (5), dhahabu lina sauti (5) ilhali neno segemnege lina sauti (5)
Hivyo ni kusema tunahesabu kila herufi ya abjadi kivyake inapopatikana au kujitokeza mara ya kwanza:
- k–i–a–t–u (5)
- dh–a-h-a-b-u (5)
- s-e-g-e-m–n-e-g-e (5)
Sauti Ghuna
Sauti hizi zikitamkwa hughuna kwa ndani. Sana sana ukiziba masikio utaisikia unapotamka sauti yenyewe mgurumo wa ndani unajitokeza.
Sauti hizi ni kama vile: b, d, dh, g, j, m, n, ng’, ny, v, w, y, z (13)
Sauti Sighuna
Sauti hizi zikitamkwa hasighuni yaani koo haitikisiki. Sana sana ukiziba masikio utaisikia unapotamka sauti yenyewe haitakuwa na mgurumo wa ndani.
Sauti hizi ni kama vile: ch, f, h, gh, l, k, p, r, s, sh, t, th. (12)
Sentensi ya ukumbusho: Sh! Chifu Seth tukupora ghala hii si-ghuna
Mwanagenzi akitaja sentensi hii atajikumbusha sauti sighuna.
Silabi Changamano
Silabi au sauti hii huundwa kwa herufi zaidi ya moja hasa konsonanti. Hutamkwa kwa pamoja na husikika zikiwa sauti moja.
Mfano katika maneno: Changamano, Muumba, kichala, dhana, ghala.
Silabi Mwambatano
Kuambatana ni kufuatana kwa mambo moja baada ya jingine. Sauti hii huundwa kwa herufi mbili au zaidi na hutamkwa moja baada ya nyingine.
Mfano katika maneno: mwambatano, mwana, kinywaji, nywele, mbwembwe. Msengwe, mfuko.
Maswali ya Alfabeti
- Herufi ch, dh, gh, ng’, ny, huitwa ___________________
- Herufi a, e, i, o, u huitwa _________________________
- Vitamkwa ambavyo huundwa na herufi sifuatazo kama ifuatavyo – ng’ + a = ng’a , z + a = za – Kwa jina moja ni ___________________
- Unapotaja herufi kama ifuatavyo – m-a-h-a-l-i – ili kuweza kuhesabu , tunasema unahesabu ___________________
- Sauti g, ny, v, z, ni sauti _________________
- Sauti f, h, l, k ni sauti ___________________
- Neno dhamana lina silabi zinazoitwa ___________________
- Neno mwao lina silabi zinazoitwa ______________________
- Neno jingine la abjadi ni ________________ au ______________
<<<<<< Majibu ya Maswali ya Abjadi >>>>>>>
Zoezi la ziada
[ays_quiz id=”2″]