Vihisishi ni maneno ya kuonyesha hisia mbalimbali za mzungumzaji. Alama ya hisi hutumika baada ya kiingizi! Tazama baadhi ya viigizi vifuatavyo vilivyopangwa kulingana na hali tofautitofauti:
Dharau
Mifano: Chub!Chup! Ebo! Khaa! Kefle! Po! Pukachaka! Nyoo! Us! Wee! Zii!
Furaha / Shangwe
Haleluyah! Ewaa! Chabaa! Oyee!
Oyaa! Huree! Shabash!
Heshima
Tafadhali!
Huruma
Jamani! Pole! Maskini!
Huzuni
Pole! Ole!
Kuchoka
Oofu!
Kuelewa
Alaa! Ahaa!
Kukanusha
Aka! Ata! Hasha! Hata! La!
Kukataa
Abadan kataan! La! Hasha!
Kamwe! Hapana! Ng‘o!
Kuitikia
Abee! Beka!
Kukemea
Ebo! Wee!
Kukubali
Barabara! Enhe! Haya! Hewaa! Hewala! Naam! Ohoo! Taib! Sawa! Taibu!
Kulaani/kukashifu
Do! Pukachaka! Zii!
Kulaani shetani
Audhubillahi!
Kuomba msaada kwa Mungu
Yarabi maskini!(msaada wa Mungu), Yarabu Stara! (ulinzi wa Mungu)
Kuomba samaha hasa unapotaka kusema jambo ambao linaweza kuudhi
Ashakum!
Kusifu Mungu
Halleluyah!
Kutia moyo
Harambee! Halumbe! Twende!
Majuto
Kama! Falaula! Lau! Laiti! Ole wangu!
Mshtuko
Aisee! Afanaleki! Alaa! Jamani!
Lo! Toba!
Mshangao
Ah! Aka! Ala! Ajabu! Cho! Do! Ewe! Haya! Kumbe! Lo! Lakwata! Masalale! Oho! Salala!
Shukrani
Asante! Alhamdulilahi!
Shaka
Eti!
Uchungu
Aa!,
Woga
Mama wee! Mungu wangu!
Maswali ya Vihisishi
Katika vikundi vya maneno uliyopewa 1-10 sema ni hali gani ya viigizi imetumika.
- Abadaan! Kamwe!
- Mama wee! Mungu wangu!
- Aka! Lakwata!
- Pole! Ole!
- Hasha! Ng’o!
- Jamani! Maskini!
- Chup! Zii!
- Do! Pukachaka!
- Barabara! Taib!
- Yarabi stara! Yarabi maskini!