Neno linalounganisha maneno, vikundi vya maneno au sentensi.
Vipo viunganishi aina kadhaa kama vile:
Viunganishi vya kulinganisha/kufananisha
Fakaifa, kaifa, kefu, sembuse, seuze
Viunganishi vya uteuzi
Ama, au, badala ya, mahali pa
Viunganishi vya kuonyesha sababu
Kwa sababu, kwa minajili, kwa maana, kwa ajili ya, kisa na maana,maadamu, kwani, madhali, kwa kuwa, ili
Viunganishi vya mambo ya mara kwa mara/mazoea
Aghalabu, mara kwa mara, ghalibu, kwa kawaida, kwa kaida
Viunganishi vya nyongeza
Aidha, mbali na, vile vile, isitoshe, hali kadhalika, fauka ya, kadhalika, licha ya, pia, zaidi ya.
Viunganishi vya masharti
Almuradi, bora, endapo, mradi, ikiwa, iwapo, taraa
Viunganishi vya uwezekano
Pengine, yamkini, yawezakana, yumkini, labda, huenda, asaa
Viunganishi vya kiini au uhusiano
Kuhusiana na, kutokana na, kwa mujibu wa, kulingana na, mintarafu ya
Viunganishi vya hali isiyo kamili/iliyo na kasoro
Bali, ila, ijapokuwa, ingawa, isipokuwa, hata ingawa, walakini, hata hivyo.
Viunganishi vya kinyume cha mambo
Hali, ilhali, lakini
Viunganishi vya kutojari
Bila ya, mingairi ya, pasi na
Viunganishi vya mkazo
Fauka ya, mbali na, isitoshe, zaidi ya,
Viunganishi vya hali yakinifu/sahihi/kweli/uhakika
Barabara, ndivyo, ni, kuntu, kwa ikrari, hakika, hasa, sawa, yakini
Viunganishi vya mfanano
Mfanano na, ja, mfano wa, mithili ya, sawasawa na
Viunganishi vya hali afadhali
Angalau, angaa, falau, walau, hata
Viunganishi vya uteuzi kati ya vingi/vya sehemu
Baadhi ya, baina ya, kati ya, katikati ya, miongoni mwa, mojawapo
Viunganishi vya sababu
Kwa ajili, kwa kuwa, kwa maana, kwani, kwa sababu, maadamu, madhali.
Viunganishi vya wakati adimu/nadra
Mara, punde, pindi