Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Insha za KCPE zilizotahiniwa tangia mwaka wa 1985 hadi 2023

Posted on By Harun Mbijiwe 2 Comments on Insha za KCPE zilizotahiniwa tangia mwaka wa 1985 hadi 2023

1985
Niliamshwa na harufu nzuri ya chakula kilichokuwa kikipikwa na mama. Mara nikakumbuka ilikuwa ni siku kuu.

1986
Nyanya alikuwa amezoea kututolea hadithi. Jioni alituhadithia kisa kimoja cha kufurahisha. Alianza hivi…

1987
Siku yangu ya kwanza kufika shuleni kwa masoma ni siku ambayo mpaka leo ninaikumbuka vizuri sana. Siku hiyo niliamshwa mapema na nikapelekwa mpaka shule. Nilipofika shuleni…

1988
Ilikuwa siku ya harambee. Mipango yote ilikuwa imekamilika.

1989
Rafiki umpendaye sana alikuja kukutembelea. Elezea jinsi ulivyompokea na kumfurahisha.

1990
Kuna faida nyingi za mtu kwenda shule kusoma. Andika insha ya kuvutia ueleze faida hizo.

1991
Andika insha juu ya:-
Elimu ni bora katika maisha yetu.

1992
Kazi ambayo ningependa kufanya baada ya kuhitimu masomo yangu.

1993
Wewe ni mmoja wa wanafunzi waliohitimu masomo yao ya darasa la nane nawe umechaguliwa na wenzako kutoa hotuba ya kuwaaga walimu na wanafunzi watakaobaki. landike hotuba hiyo.

1994
Andika insha itakayomalizia kwa:-
…nilihisi bibaya sana nilipogundua kuwa hiyo ilikuwa ndoto tu.

1995
Mwandikie barua rafiki yako anayeishi mbali ukimwelezea yailyotokea pale unapoishi tangu mwaka jana.

1996
Andika insha itakayomalizika kwa maneno:-
………. Ndipo nikaamini kwamba haraka haraka haina baraka.

1997
Andika insha juu ya mawaidha yaliyotolewa na mgeni wa heshima siku ya utoaji zawadi shuleni mwenu.

1998
Nilipozinduka nilijikuta nimelala chini ya mti, katikati ya msitu mkubwa uliojaa wanyama wa kila aina.

1999
Endeleza kisa hiki.
Ulikuwa usiku wa manane niliposikia mayowe.

2000
Andika insha juu ya:

Mungu hamsahau binadamu wake.

2001
Umeshinda shilingi milioni moja katika mchezo wa bahati nasibu. Eleza utakayoitumia pesa hizo.

2002
Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wenzako kuhusu umuhimu wa kudumisha usafl wa mwili na mazingira.

2003
Siku yenyewe ilikuwa ljumaa. Nakumbuka vizuri sana namna baba alivyoingia nyumbani endeleza.

2004
Andika insha juu ya kichwa kifuatacho. “Mchumia juani hulia kivulini.”

2005
Malizia insha yako kwa….Nilishangaa nisiweze kuamini kuwa nilikuwa nimeepuka hatari hiyo. Moyoni nilimshukuru Mungu kwa kuniokoa.

2006
Malizia kwa:-
Sherehe zilipomalizika nilirudi nikiwa na furaha tele.

2007
Rafiki yako amehamishwa na kujiunga na shule nyingine. Mwandikie barua ukimweleza maendeleo yako tangu mlipoachana.

2008
Anza kwa:
Wingu kubwa jeusi lilitokea upande wa mashariki. Baadaye matone mazito mazĂ­to….

2009
Usiku wote sikupata hata lepe la lausingizi. Niliwaza na kuwazua namna siku ambayo ilifuata ingekuwa …

2010
Malizia kwa maneno haya.
..kwa kweli niligundua kuwa Mungu akifunga nafasi hii hufungua kwingine.

2011
Mwandikie rafiki yako barua ukimshauri kuhusu namna ya kujiandaa vyema kwa mtihani wa KCPE.

2012
Anza kwa:
Machozi ya furaha yalinitiririka; sikuyatarajia haya…..

2013
Wewe ni kinara wa wanafunzi shuleni. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wenzako kuhusu umuhimu wa kudumisha usafi.

2014
Malizia kwa maneno haya:
…. huyo alikuwa ndugu ambaye kamwe sitaweza kumsahau.

2015
Malizia kwa maneno haya:
Hakika nilikuja kuamini kwamba mtu akitia bidii katika jambo, hata liwe gumu vipi, hatimaye hufaulu.

2016
Anzia kwa maneno haya.
Ufanisi wa mwanafunzi katika masomo humtegemea yeye…..

2017
Mwandikie rafiki yako barua ukimshauri kuhusu mambo ambayo anaweza kufanya ili kujiimarisha katika masomo.

2018
Malizia kwa:
…… Hapo ndipo niligundua kwamba ndugu, hata akiwa mbaya vipi, hawezi kukuacha wakati wa shida.

2019
Maliza kwa:
….. Hakika nilikuja kugundua kwamba ni muhimu kuwazia hatari ya kufuata yale ambayo marafiki wanatenda.

2020
Mwandikie barua rafiki yako ukimweleza kuhusu namna anavyoweza kutumia likizo yake vyema kujinufaisha.

2021
Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
……. Tulikutana tena baada ya tukio hilo la wema. Ulikuwa umepita muda mrefu lakini baadaye nilimshukuru.

2022
Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
Habari hiyo ilipofikia, tulifurahi sana.

Ninawataka kila la heri watahiniwa wote, Jalali awajalie baraka belele.

Post Views: 317
Utahini wa Insha KCPE

Post navigation

Previous Post: Tashdidi
Next Post: Mjadala

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme