Mwanafunzi aelewe kuwa kifungukate au kiasho hutahini mambo kadhaa ya sarufi, kusikiliza na kuzungumza, msamiati na ufahamu wa maendelezo tofautitofauti ya maneno ambayo wakati mwingine huendelezwa visivyo. Mambo haya yote huwa yanajitokeza lakini linalochukua sehemu kubwa ni sarufi.
Mwanafunzi anaposoma kifungukate anapaswa aangalie:
Nyakati
Kifungu kimeandikwa kwa wakati gani kwa mfano:- li wakati uliopita, na wakati uliopo, ta wakati ujao nk.
Ngeli
Atazame aaone ni ngeli gani zimetumika katika kila sentensi ili aweze kuteua viambishingeli vinavyofaa. Km. Mama alikuwa ____1_____ sokoni magari ____2___ kwetu nyumbani. Majibu yanapaswa kulenga nomino mama na magari ambazo ni nominokuu katika sentensi.
Virejeshi
Mwanafunzi ajue kuwa virejeshi hutahiniwa kwa sababu huleta msisitizo katika sentensi husika au kurejelea nomino fulani katika sentensi yenyewe.
Tazama: Kitabu kilichokuwa kikizungumziwa ni hiki. Rejeshi o kati imetumika kuleta msisitizo na kuifanya sentensi iwe sawa kisarufi.
Nafsi
Mwanafunzi aajue wahusika wanaozungumziwa ni kina nani. Ajue atarejelea mtu wa kwanza, wa pili au wa tatu. Km. ‘_____ kwenu kesho nikuone.’ Karani alisema. Nikitumia vijalizo(atakuja, nitakuja, wangekuja) jibu sahihi ni nitakuja kwa sababu mzungumzaji yu katika nafsi ya kwanza umoja na kiambishi ni kinapaswa kutumika.
Msamiati
Mwanafunzi ajue na atambue msamiati uliotumika katika kifungu. Kwa mfano shuleni hatuna watu na nyumba bali wanafunzi, ofisi, walimu, walinda lango, bwalo, madarasa, ofisi, walimu, madaftari nk.
Shambani atapata mboji, makoongo, matuta, tikitimaji, pilipili mboga, pilipili hoho, tololi, nk
Maendelezo
Maendelezo ya majina yanayoendelea visivyo hutahini wa sana katika kifungukate. Mifano: maakuli na mankuli, maandazi na mandazi, kiamshakinyua na kiamsha kinyua, makazi na makaazi, kwa sababu na kwasababu, dhahabu na thahabu, ghorofa na gorofa nk.
Viunganishi
Maneno ya kuunganishia sentensi hutahiniwa sana katika kifungukate. Mwanafunzi aelewe maana na visawe vya viunganishi ili iwe rahisi kwake kujibu maswali atakayokutana nayo. Mfano: sembuze au seuze, fakaifa, kefu huonyesha kulinganisha mambo mawili la kwanza likiwa ngumu kuliko la pili.
Katika sentensi:- Umemla mbuzi mzima seuze sungura.
Kusikiliza na kuongea
Sehemu hhii hutahini sehemu mbalimbali za kusikiliza na kuongea. Mwanafunzi ajikakamue kuelewa kwa kiwango kikubwa:-
- Tashibihi
- Methali
- Nahau
- Semi
- Visawe
- Vitawe
- Vitate nk