Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Kuponea Chupuchupu

Posted on By Harun Mbijiwe 6 Comments on Kuponea Chupuchupu

Andika isha isiyopungua sahifa moja u nusu kwa kutumia mdokezo ufuatao: … Ninamshukuru Dayani kwa kuninusuru. Hadi leo sijaona lango la nyumbani.

KUPONEA CHUPUCHUPU

Ninadhukuru kitendo cha dhuluma, wakati na siku hiyo kama jana. Nilitoka shule nikiwa na roho nzito mithili ya nanga. Sikufahamu wala kumaizi lililokuwa mbele yangu. Jambo lililonitia moyo ni kuwa mimi ni mcha Maulana. Waja wa dini waliamba yaliyofichwa ni ya Dayani na yaliyo wazi ni yetu. Nilijipa moyo na kuendelea na safari yangu kuelekea mastakimuni. Huku njiani niliendelea kumwomba Rabuka aniondolee mzigo uliokuwa mtimani. Niling’amua na kujua kwamba mcha Mungu si mtovu aidha Mungu si Adhumani.

Nilipokaribia kitendeni niliona moshi ukivuka kwetu kama tanuri. Pavukapo moshi pana moto waambao waliamba. Sikufiria zaidi lakini nilivyokaribia chengoni ndivyo manyezi yalinivika kama joho. “Sikuacha mambo haya au matayarisho fulani , imekuaje?” Nilijiuliza na kujisaili. Kweli usilolijua ni usiku wa giza.

Kufika tu niliingia moja kwa moja hadi pale nina alipokuwa. Nilimwuliza lililokuwa la mno. Hakunijibu wala kunena nami. Akanitazama kwa huzuni na kusema, ‘Utajua tu mwanangu.’ Nikajua kwamba mambo ni kangaja huenda yakaja. Roho yangu ikafifia na kukosa amani. Nikajisikia mfu.

Kule nje wazee pamoja na baba yangu walikuwa chini ya mkuyu uliyokuwa upande wa yamini wa boma letu wakichapa mtindi. Upande wa Matlai karibu na zeriba wanawake waliokuwa wakijikongoja kwa mikongojo walikuwa  wameketi na kutuama. Kila kikundi kilikuwa kikinong’onezeana chini kwa chini.

Nilikuwa nimeshavunja ungo mwaka huo tu. Nilichanganyikiwa sawasawa na mja aliyekutana na mizuka. Nikatamani kulia nikacheka. Nikatamani kucheka nikalia kwikwikwi. Yapi haya? Kama ni wewe ungefanya nini? Nilipitia nyuma ya ‘manyatta’ ya mama huku nikitetemeka kama muwele wa malaria. Mawazo yalinisonga na kunizinga kichwani kama mashua katika bahari iliyo na zingo. Kwa ikrari, dunia ni rangi rangire aidha ni dunia huzunguka kama pia.

Nilijikuta katika chumba changu kidogo nikilia kwikwikwi. Mwili wangu ukaniregea. Miguu yangu ikashindwa kustahimili uzito wa mwili wangu. Nikaanguka na kugaagaa kama nyoka aliyekaribia kwenda jongomeo. Nikatamani ardhi ipasuke inimeze nili hai.

Baada ya kukaa pale kwa muda, nikakumbuka Dayani Mkawini faraki na ardhi. Nikamlilia anionyeshe yaliyokuwa yakifanyika. Wakati huu giza lilikuwa limeanza kutaanda na kufunika ardhi kama zulia. Jua lilikuwa limeshatupa mkono wa buriani kitambo. Mama akaja chumbani pangu na kunikumbatia. Nikalilia kifuani pa nina naye akalia. Tukliliana kama vilebu. Baadaye akatua roho na kunifahamisha kuwa mama yake baba ambaye ni nyanya yangu alikuwa amewaita wanakijiji na akraba kwa sababu yangu ili kuonana na ngariba. “Kukeketwa wasema?” Nikashtuka nusura nizirai. Moyo ukanipapa na kuniturutika. “Niliyoyaogopa zaidi yamenijia. Nyanya amenifikilia udhalimu!” Nikalia maozi yakavimba. Kukuli mithaki, kilio si dawa.

Baada ya mama kunituliza roho nikaitika na kukubali shingo upande. Wakati huo nyanya alikuwa aefika mlangoni na alikuwa tayari kusikiliza wazo langu. Nikasema kuwa sikuwa na shida kwa sababu nilijua yajapo yapokee. Wakati huu, nilikuwa nikitetemeka kama unyasi utetemeshwao na upepo msimu wa kipupwe. Nikatoa huku nikitilia kule. Mawazo yakanisinga na kunizonga si haba.

Somo akatayarisha vifaa na wote wakaanza nyimbo za kunishukuru. Kwangu zilikuwa za kunikehi na kunibeua, maana kilindini nilijua na kufahamu hilo lizingewezekana.nilikaa nikituma dua na kusali kila dakika angalau Rabuka anipe wazo.

Wakati huu kila jambo lilikuwa shwari bila shari.  Kila chombo kilitandazwa mbele yangu. Nikatua libasi zangu. Nikapewa shuka nikalie. Wakati huu nilikuwa nikitetemeka kama aliyeona mizuka. Kungwi akaomba apewe wia zaidi ili aweze kufanya gange yake.

Mara tu wimbo ulipopaa hewani, la ibra lilitendeka. Taa ya kibatari iliyokuwa juu ya mhimili ilianguka na kupasuka ‘Twaf!’ Sote tuliruka nje. Mimi na shuka yangu! Mafuta ya taa yakatapakaa na moto ukahinikiza chumbani. Ukemi ukapaa nami nikasema mguu niponye, nilipopata tu nafasi. Kabla ya kuku kumeza punje au paka kunawia mate nilikuwa kilomita kadhaa kutoka kwetu. Kina mama na kuzima moto mimi siti Sitorudi na pujo mguu niponye. Nilipiga breki nyumbani kwa daktari Torome huku nikiwa na shuka tu. Alinichukua na kesho yake tukaandamana naye kwenye shule ya kuwaauni walionusurika ukeketaji. Ninamshukuru Dayani kwa kuninusuru. Hadi leo sijaona lango la nyumbani.

Post Views: 235
Insha Mbalimbali

Post navigation

Previous Post: Mjadala
Next Post: Masa yanayofanywa sana katika uandishi wa insha

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme