Andika insha ya kusisimua kuhusu mama yangu mpendwa.
MAMA YANGU MPENDWA
Mama yangu anaitwa Zaibaki Zuhura. Yeye ni mzaliwa wa Pembembili nchini Bahari. Ni mtoto wa nne wa bwana na Bi. Harusi Kipepeo ambao walikuwa waanzilishi wa chama cha mapinduzi miaka ya sabini.
Mama yangu mpendwa amezaliwa pamoja na umbu zake watano. Karibia Zubaka, Ndodi Kipau, Rukia Hamadi, Gagara Rufani na Changamka Bitimarembo ambaye ni mnuna wao.
Nina yangu ameumbwa akaumbika. Sura yake jamala hupendeza ghaya. Utadhani ni hurulaini wa peponi ameshuka kutoka kwenye falaki. Viungo vyake vyote huona na kuwiana kwa ustadi na urembo usiomithilika. Mkawini ampe nininamnyime nini?
Rangi yake ya kahawia hafifu humfanya aonekane mlimbwende na mrembo zaidi. Meno yake meupe pe hujitokeza na kujitetea kila apigapo tabasamu. Nayo hujalizwa na mkubaliano wa macho yake meupe kama maziwa.
Yeye ni mfanyabiashara mashuhuri jijini Mapendo. Aidha ni mkurugenzi mkuu katika kampuni yake inayoitwa CRANES ambayo hushughulikia mauzo ya vitu vya mapambo. Kampuni yenyewe imeshakuwa kampuni nambari moja katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu mauzo yanayolenga mwananchi wa kawaida.
Mama yangu ni msomi. Hii ni kwa sababu ameisha hitimu na uzamifu katika chuo kikuu Mazungumzo. Amesoma mambo ya biashara na uchumi. Hili linamwezesha kufanya gange murua katika uwanja mpana wa biashara.
Mama huamini umoja ni mguvu na utengano ni udhaifu. Ameungana na wanajamii pamwe na wanakijiji wa Tibwirika kilichoko Pembembili kuunda vikundi vya kina mama. Vikindi hivi husaidiana kwa kuweka vitegauchumi mbalimbali. Mama hufurahia anapowapa mauzia na kuwaongoza katika mambo mbalimbali ya kujinufaisha. Kweli, lakini kwenhako hisani hurudi hisani.
Mama ameishaolewa na baba yangu. Waliona a wakisomea katika chuo kikuu na wakapendana na kushirikiana kama kiko na digali. Tangu wakati huo wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miongo miwili. Wamealikwa na watoto wanne. Mimi ni mzaliwa wa tatu.
Mama ni mpishi hodari. Anapenda kupitia ka mapishi kama vile pilau, wali wa nazi, matobosha, kitoweo cha nyama, samaki, kuku, chapati na mengineyo. Chakula akipendacho zaidi ni wali kwa kuku.
Anapenda kuvaa mavazi ya meli mpya. Viatu vyake vya mchuchumio haviachwi nyuma kama koti. Yeye huvaliwa mkufu wa dhahabu shingoni, bangiri za dhahabu, na herini za madini mengineyo. Hupenda kutumia kibano nyweleni ambapo huishia nywele yake ndefu ambayo ninaifananisha na singa.
Nina yangu ni mpenzi wa michezo hasa mchezo wa kandanda. Yeye ni shabiki sugu wa timu ya nyumbani KIPANGA. Wakati mwingine akichapa kazi pale mastakimuni hasa wikendi, yeye huvaliwa jezi nambari 5 mgongoni.
Mama anapenda kufuga wanyama. Anapenda kilimo na kazi za nyumbani. Yeye si mzembe. Anajua na kufahamu, ajizi nyumba ya njaa na mtegemea cha nduguye hufa maskini. Hujitegemea yeye mwenyewe.
Kutokana na bidii ya kazi yake, amejinunulia shangingi la kifahari. Amenunua nyumba mjini Beramu. Ameweza kujengea wazazi wake jumba kama kasri. Amefanya maendeleo mengi kijijini Tibwirika.
Nnampenda mmama. Yeye ni mtu wa kupigiwa mfano si kijijini tu, bali pia kijini.