Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Masa yanayofanywa sana katika uandishi wa insha

Posted on By Harun Mbijiwe 6 Comments on Masa yanayofanywa sana katika uandishi wa insha

Sarufi

Kuakifisha nomino mahususi visivyo

Nomino mahususi huanza kwa herufi kubwa lakini wanafunzi wengi huziandika kwa herufi ndogo kama vile:-

  • mungu – Mungu
  • kimathi – Kimathi
  • mombasa – Mombasa
  • kenya – Kenya
  • ziwa Nakuru – Ziwa Nakuru

Kuandika kivumishi kabla ya nomino.

Mwanafunzi aelewe kuwa kivumishi huelezea zaidi kuhusu nomino na hakiwezi kuja kabla ya nomino. Km.

  • Huyo mtu – mtu huyo
  • Hiyo shule – shule hiyo
  • Hayo mayai – mayai hayo
  • Hicho kiatu – kiatu hicho

Ngeli na viambishi vyazo.

Mwanafunzi asitumie viambishingeli tofauti na nomino kuu katika sentensi. Atumie ngeli na viambishi vyake ipasavyo. Km.

  • Pua linaniuma – pua inauma
  • Alipigwa kichwani mwake – alipigwa kichwani
  • Darasa yake ni ile – darasa lake ni lile

Wingi usiokubalika

Yapo maneno ambayo hayawezi kubadilika katika umoja na wingi. Mwanafunzi ajue kupachika kiambishi cha kuonyesha wingi katika maneno hayo ni kupotosha maendelezo. Mifano:

  • Madawa ya kulevya – dawa za kulevya
  • Masaa – saa
  • Mapua yanauma – pua inauma
  • Mashule yamefungwa – shule limefungwa
  • Makaratasi yalipeperushwa na upepo – karatasi zilipeperushwa kwa upepo

Matumizi ya kistari kifupi

Ukanushi

Ukanushi wa viambishingeli
  • Ngeli A – Wa hukanushwa kwa ha na hawa
  • Ngeli Li – Ya hukanushwa kwa hali na haya
  • Ngeli U – I hukanushwa kwa hau na hai
  • Ngeli Ki – Vi hukanushwa kwa haki na havi.
  • Ngeli I – Zi hukanushwa kwa hai na hazi. Nk
Ukanushi wa viambishinafsi
  • Kiambishi ni nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa si. Mfano ninapenda – siendi
  • Kiambishi tu nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa hatu.
  • Kiambishi u nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa hu.
  • Kiambishi m nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa ham.
  • Kiambishi a nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa ha.
  • Kiambishi wa nafsi ya kwanza umoja hukanushwa kwa hawa.

Maendelezo au hijai

Kutenganisha vifungutenzi

Mwanafunzi asitenganishe vitenzi au vifungutenzi kwa sababu humwadhiri katika msamiati. Alama zake hupunguzwa kwa sababu hiyo. Mifano ni:

  • Yanayo tupa – yanayotupa
  • Tunapo soma – tunaposoma
  • Wanavyo imba – wanavyoimba
  • Kinacho tisha – kinachotisha
  • Tulipo amka – tulipoamka

Kutenganisha vielezi radidi au vikariri.

Makosa haya huadhiri misamiati pia. Mwanafunzi aelewe kuwa vielezi radidi huandikwa kama neno moja.

  • Ovyo ovyo – ovyoovyo
  • Aste aste – asteaste
  • Pole pole – polepole
  • Hobela hobela – hobelahobela
  • Juu juu – juujuu

Kutenganisha nominoambata

  • Mwana hewa – mwanahewa
  • Askari polisi – askaripolisi
  • Mwana sesere – mwanasesere
  • Kiangaza macho – kiangazamacho
  • Kiinua mgongo – kiinuamgongo

Kuongezea herufi katika neno

  • Makaazi – makazi
  • Masikini – maskini
  • Ekisrei – eksrei
  • Rundi nyumbani – rudi nyumbani
  • Kanyanga – kanyaga
  • Chemichemi – chemchemi
  • Bibilia – Biblia
  • Lisaa – saa

Kutoa herufi katika neno

  • Gorofa – ghorofa
  • Mandazi – maandazi
  • Makuli – maakuli
  • mankuli – maakuli
  • Sherekea – sherehekea
  • Maskio – masikio
  • Malum – maalum
  • Mnyonyoko wa udogo – mmomonyoko wa udongo

Masa ya herufi tata

  • Panguza – pangusa
  • Guruguza – gurugusa
  • Guza – gusa
  • Chamba – shamba
  • Roli – lori

Kuunganisha maneno

Yapo maneno mengi hasa nomino, viunganishi pamoja na vitenzi ambayo wanafunzi huandika kama neno moja badala ya maneno mawili. Mifano:

  • Mwalimumkuu – mwalimu mkuu
  • Kwasababu – kwa sababu
  • Kwanini – kwa nini
  • Kwakuwa – kwa kuwa
  • Namimi – nami au na mimi
  • Nayeye – naye au na yeye
  • Ilikucheza – ili kucheza
  • Ilituende – ili tuende

Maendelezo mabaya katika utohozi

Maneno yaliyotoolewa huwa yameandikwa kutoka katika lugha ngeni kwa kubadilisha katika Kiswahili kuifuata sauti zile zile sa lugha husika.

  • Ambulanci – ambulansi
  • Geograhia – Jiografia
  • Siyansi – Sayansi
  • Technologia – tekinolojia
  • Televisioni – televisheni
  • Secondari – sekondari
  • Radio – redio
  • Oxygeni – oksijeni
  • Kabondioxidi – kabonidayoksaidi
  • Millioni – milioni

Matumizi ya msamiati usio vidahizo

Hata kama Kiswahili kinakua, mwanafunzi ajue kuwa maneno yasiyotiwa kwenye kamusi yaani vidahizo asiyatumie. Yapo majina kadhaa ambayo yanaibuka kutoka kwa lugha ya mtaani au katika lahaja za Kiswahili ambazo hasijakubalika . Mifano ni kama vile:

  • Kaski
  • Ndemi na mathathi
  • Yaumu
  • Bimithili
  • Tamadhali

Wingi na umoja wa nomino fulani spesheli

Yapo majina ya ngeli A – Wa ambayo huchukua wingi unaotatiza yanawabwaga wanafunzi mno. Mifano:

  • Nyani wamelala – manyani wamelala.
  • Seremala wanashona manguo – maseremala wanashona nguo.
  • Bata wameruka – mabata wameruka.

Kubadili fani za lugha

Methali

  • Siku za mwizi ni makumi manne.
  • Siku njema huonekana mafungulia nyama.
  • Siku njema huonekana mafungulia bakari/ Ng’ombe

Kutumia majina ya ushairi

  • Abu
  • Abyadhi
  • Bakari

Tanbihi;

Yapo masa zaidi japo nimeyataja machache. Unapoendelea kupitia insha yako pamoja na mdarisi u mwanafunzi wako, utapata kuwa yatajitokeza zaidi. Uliza mwalimu kila kosa alilokistari kama huelewi ili ujue ni kwa nini amefanya hivyo.

Post Views: 178
Mawaidha ya Ufundishaji

Post navigation

Previous Post: Kuponea Chupuchupu
Next Post: Hotuba

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme