Dondoo au mdokezo ni insha ambayo mtahiniwa hupewa mwanzo au mwisho wa hadithi. Mtahiniwa huhitajika kutoa kisa kinachodhihrisha na kulenda maudhui yanayoafikiana na mdokezo ule aliopewa.
Mwanafunzi anahitajika kuwa na utangulizi ulio na mvuto. Mwili wa insha ulenge maudhui kwa kina. Ahitimishe kwa wazo la kukumbukwa au wasia mwafaka.
Mwanafunzi anahija kuangazia mambo kadhaa ili alenge maudhi barabara kwa mfano:
- Ashughulikie wakati.
- Ashughulikie mandhari.
- Aangalie na ateue wahusika walioko.
- Ashughulikie tukio au matukio kwa kina.
- Ashughulikie hisia.
- Achambue hoja zake kwa kina katika kila aya.
- Atumie lugha tasfida na iliyo na maadili.
Tazama mfano ufuatao kwa kubonyeza hapa: Insha ya dondoo