Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiriwa na jamii kuwa kweli na unaotumiwa kufumbia au kupigia mfano na huwa umebeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. ( Maelezo kutoka katika Kamusi ya TUKI uk 240)
Kwenda na wakati
- Aendaye kisimani wa kwanza hunywa maji maenge.
- Chuma kiwahi kingari moto.
- Ivute ngozi ingali mbichi.
- Kambare mkunje angali mbichi.
- Samaki mpatilize angali mbichi.
- Tikiti ni moto wa kwanza.
- Udongo upatilize ungali maji.
- Udongo uwahi uli maji.
Thadhari dhidi ya tamaa
- Bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi.
- Chako ni chako cha mwenzio si chako.
- Fuata nyuki ukafie mzingani.
- Mkate mkavu wa nyumbani ni bora kuliko nyama ya pengine.
- Mla kwa miwili hana mwisho mwema.
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
- Mtaka yote hukosa.
- Mwangata mbili moja humponyoka.
- Njia mbili zaumiza.
- Njia mbili zilimshinda fisi.
- Tamaa ilimwua fisi.
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Usiache kunanua kwa kutega.
- Usisafilie nyota ya mwenzio.
Umoja na ushirikiano
- Jifya moja haliinjiki chungu.
- Ukuni mmoja hauwaki mekoni.
- Kichango ni kuchangizana.
- Kidole kimoja hakivunji chawa.
- Kijiti kimoja hakisimamishi jingo.
- Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
- Kofi hazilii ila kwa viganja viwili.
- Mafiga mawili hayaivishi chungu.
- Mkataa wengi ni mchawi.
- Mkono mmoja hauchinji ng’ombe.
- Mkono mmoja hapambi ngoma.
- Mkono mmoja haushindi vita.
- Mkono mmoja haubebi.
- Mtu ni watu.
- Nguzo moja haijengi nyumba.
- Nyege ni kunyegezana.
- Tembe na tembe huwa mkate.
- Ukiujua huu hujui ule.
- Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
- Vitanga vya mkono hunawishana.
- Watu ni kikoa.
- Wawili si mmoja.
Nasaha ya kutia bidii
- Mchumia juani hulia kivulini.
- Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
- Zohali ni nyumba.
- Ajizi ni nyumba ya njaa.
- Auguaye huaguliwa.
- Bahati ni chudi.
- Kawia ufike.
- Kilicho baharini kakingoje pwani.
- Mgagaa na upwa hali wali mkavu.
- Mtaka cha mvunguni sharti uiname.
- Mvumilivu hula mbivu.
- Mwana mtukutu hali wali mtukutu.
- Mwenye shoka hakosi kuni.
- Ukitaka la waridi sharti udhurike
Tahadhali dhidi ya kuhadaika kwa sura ya nje
- Vyote viowevu si maji.
- Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.
- Kizuri hakikosi ila.
- Mchele haukosi ndume.
- Penye urembo ndipo urimbo.
- Sihadaike na rangi tamu ya chai ni sukari.
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
- Uzuri wa kuyu ndani mabuu.
- Vyote ving’aavyo si dhahabu.
- Nasaha ya kutokata tamaa
- Baada ya dhiki faraja.
- Kenda karibu na kumi.
- Mla cha uchungu na tamu hakosi.
- Mvumilivu hula mbivu.
- Penye nia na milango ipapo.
- Penye nia pana njia.
- Taabu ya leo ni furaha ya kesho.
- Tembe kwa tembe huwa mkate.
- Tone kwa tone huwa mchirizi.
- Umemla ng’ombe mzima husishindwe na mkia.
- Zito hufuatwa na jepesi.
- Wimbi kali hufuatwa na shwari.
Tahadhari dhidi ya kucheka kasoro za wengine
- Ajabu ya kibogoyo kumcheka mapengo.
- Ajabu ya kondoo kucheka kioo.
- Ajabu ya ngamia kucheka nundu ya ng’ombe.
- Ajabu ya kipofu kumcheka chongo.
- Nyani haoni kundule.
- Nyani huchekana ngoko.
Nasaha ya kufuata udugu
- Damu ni damu si kitarasa.
- Cha ndugu huliwa na ndugu.
- Damu ni nzito kuliko maji.
- Isipowasha hunzaye.
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa naye.
- Ndugu chungu jirani mkungu.
- Ndugu mbaya humshinda rafiki mzuri.
- Ndugu mtambie usimkalie.
- Ndugu mui heri kuwa naye.
- Ndugu ni kufaana si kufanana.
- Udugu wa nasi hukutania pakachani.
- Wa kuume haukati wa kushoto.
Nasaha ya kutenda wema
- Jaza ya hisani ni hisani.
- Kumpa mwenzio si kutupa.
- Kwendako hisani hurudi hisani hakurudi nuksani.
- Mtenda jamala hulipwa jamala.
- Wema hauozi.
- Tenda wema huende zako.
Tahadhari dhidi ya maringo
- Usione Kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
- Pavumapo palilie si kazi kudamirika.
- Aliye juu mngojee chini.
- Mpanda ngazi hushuka.
Tahadhari dhidi ya kudharau ulivyo navyo
- Usione tanga la nguo ukasahau la miyaa.
- Baya baya lako si jema la mwenzio.
- Bura yangu siibadili na rehani.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Usidharau dafu embe ni tunda la msimu.
- Usile na sahani ukasau bunguu.
- Usisahau ubaharia kwa sababu ya unaodha.
Nasaha ya kuwa na subira
- Haraka haraka haina Baraka.
- Kakaka haina Baraka.
- Kawia ufike.
- Mbio za kasa si mbio lakini humfikisha aendapo.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
- Mstahimilivu hula mbivu.
- Mnywa maji kwa pupa kiu yake i pale pale.
- Mvumbika mbichi hula mbivu.
- Mwenda pole hajikwai.
- Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
- Asubiriaye hajuti.
- Polepole ya kobe humfikisha mbali.
- Poepole ndio mwendo.
- Samba mwenda kimya ndiye mla nyama.
- Subira huvyaa mwana mwema.
- Urumi haikujengwa kwa siku moja.
Tahadhari dhidi ya kudharau waliokufaidi
- Mchana ago hanyeri huenda akauya hapo.
- Usimcheke mamba kabla ya kuvuka mto.
- Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
- Visima vya zamani havifunikwi.
- Daraja lililokuvusha usilitukane.
Anayejua jambo vizuri ni aliye karibe nalo
- Siri ya mtungi aijuaye kata.
- Aibu ya maiti aijuaye ni mwosha.
- Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti.
Kutosikia mawasia na majuto
- Asiyeangalia huishia ningalijua.
- Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
- Asiyesikia huishia ningalijua.
- Asiyesikia husafiria mtumbwi wa mfinyanzi.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Asiyesikia la wakuu hufikwa na makuu.
- Kiburi majuto.
- Kilio si dawa.
- Maji yakimwagika hayasoleki.
- Majuto ni mjukuu mwisho huja kinyume.
- Mdharau mwiba huota tende.
- Msiba wa kujitakia hauna kilio.
- Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole.
- Palipo wazee hapahabiki jambo.
- Radhi ya wazee ni fimbo kubwa kwa mwanadamu.
- Sikio halipwani kichwa.
- Mkataa pema pabaya pamwita.
Tahadhari dhidi ya kujiusisha na mambo yasiyokuhusu
- Aliye kando haangukiwi na mti.
- Samli ya pemba haimpati mtu macho.
- Pilipili iliyo shambani yakuashiani.
Akiba
- Akiba haiozi.
- Akiba ni iliyo kibidoni.
- Akiba si mbi ingawa ya kumbi siku ya kivumbi katia motoni.
- Hakuna hakiba mbovu.
Tahadhari kwa kuzuia wengine wasinufaike
- Jivu usilolilalia usilipigie jibwa.
- Mavi usiyoyala wayawingiani kuku.
- Mtama usioula wauwingiani ndege.
- Mzigo u kichwani kwapa lakutokeani jasho.