Nahau ni nini?
Hili ni fungu la maneno lililo na maana ambayo haotokani na maana ya aneno yanayounda fungu hilo. mwanafunzi anahitajika kujua kuwa mafungu haya yanapotumika katika ulumbi humpa mzungumzaji hadhi na kuonekana mwenye utawala katika maongezi. Katika uandishi humsaidia mtahiniwa kupata alama zaidi katika msamiati ambao huwa ni jumla ya alama 12. Tazama mifano ifuatayo:-
A
- Akraba kuukeni – jamaa wa upande wa mama
- Akraba kuumeni – jamaa wa upande wa baba.
- Akrabu kusini/Akrabu Kaskazini/Akrabu Magharibi/Akrabu Mashariki – Upande wa kusini/Upande wa Kaskazini/Upande wa Magharibi/Upande wa Mashariki
- Alfa na Omega – mwanzo na mwisho.
- Alfajiri mbichi – kati ya saa tisa na saa kumi asubuhi.
- Alika vita – chochea vita.
- Ambulia patupu – feli katika jitihada fulani au kosa kufanikiwa.
- Andaa meza – kutayarisha chakula
- Andika jicho – kondolea mtu macho.
- Andika meza – tayarisha kwa kuweka vyombo mezani wakati wa Chakula.
- Angaza macho – tazama au angalia Mahali pamoja.
- Angika roho – kuwa na hofu au wasiwasi.
- Angua kicheko – cheka kwa sauti.
- Anguka kitakotako – sambaratika au haribika kwa jambo fulani.
- Angukia pakavu/patupu – kosa kufaulu
- Angusha karamu – andaa sherehe
- Angusha uso – ona aibu
- Arusi ya mzofafa – arusi kubwa ya kutajika.
- Arusi ya ndovu kumla mwanawe – arusi kubwa.
- Asa mtu – kumpa mtu Mawaidha.
- Ashiki wa jambo – anayependa sana jambo fulani.
- Awa damu –tokwa na damu.
- Awa jasho – tokwa na jasho.
B
- Bahari kubwa – matatizo au shida nyingi.
- Bakua kofi – gonga hwa kiganja cha mkono.
- Banwa na kapu – ona njaa.
- Baraka za kasole – Baraka kwa wingi.
- Benua kidari – kujionyesha; kujigamba; kujiringa
- Biwi a ghubari – mvurugiko wa mambo au vumbi nyingi.
- Bonge la mtu – mtu mnene au mkubwa.
- Bukua siri – fichua siri.
- Bure bilashi – bila sababu.
- Bwaga wimbo – anzisha wimbo.
C
- Chai ya mkandaa – chai isiyo na maziwa au chai kavu.
- Chana mbuga – toroka
- Chana mbuga – toroka.
- Chapa miguu au milundi – tembea; enda kwa miguu.
- Chapa mtindi/maji – kunywa pombe kwa wingi.
- Cheza kayaya za chini kwa chini, kutia kiwi, paka mafuta kwa tako au kwa mgongo wa chupa, – danganya; hadaa mtu.
- Chezea sega la nyuki/chokoza mavu – cheza na jambo hatari.
- Choma ini – umiza moyo kwa hasira.
- Chuna ngozi – ondoa ngozi
- Chungulia kaburi/mava – karibu kufa.
D
- Dabuka uso – furaha; changamka.
- Daka la mwana – mtoto aliyelelewa vizuri.
- Damu ya nzi – damu kidogo.
- Dodosa maneno – sema kwa kusitasita.
E
- Enda cheguchegu – tembea huku ukichechemea.
- Enda jongomeo, kwenda kuzimuni, kufuata njia ya marahaba, kupungia dunia mkono wa buriani, kutangulia mbele ya haki, kuipa dunia kisogo, kata kamba, koma moyo – Kufa.
- Enda mrama, mambo kwenda shoto, mambo kwenda upogo, mambo kwenda segemnege, mambo kutumbukia nyongo – kuharibika kwa jambo au mambo.
- Enda msalani – kwenda chuoni.
G
- Ghafla bin vuu – tendeka labda bila kutarajiwa.
- Gonga mwamba – kutofanikiwa.
I
- Ima fa ima – kwa vyovyote vile.
- Ingia topeni – kwama katika kutenda jambo; shindwa kuendelea.
- Inshallahu taala – Mungu mtukufu akipenda.
K
- Kata kamba – kuaga dunia
- Kata kiu, kukonga roho – kumaliza kiu ya maji.
- kujifunga nira, kujifunga masombo, kujifunga kibwebwe – kufanya bidii.
- Kujipa moyo – kujiliwaza
- Kula yamini – apa
- Kuwa na ndege mzuri, kushukiwa na nyota ya jaha, kuwa na mkono mzuri – kuwa na Bahati
L
- Lala kigogo – lala usingizi mzito.
- Lambata/ saka wanyama – winda.
- Laza damu, kuwa kupe, kuwa chaza, kuwa na mkono mzito – kuwa mzembe.
P
- Pata jiko, kuasi ukapera, kufunga ndoa/nikahi/nikaha, kufunga pingu za maisha – kuoa.
- Pata nafuu, kuona ashekari, kuona afueni – kuwa katika hali ya kukaribia kupona.
- Piga darubini – kufanya uchunguzi
- Piga hatua – kuendelea mbele
- Piga mbio – kimbia
- Piga moyo konde – kujituliza/kujiliwaza
- Pigwa kalamu – kufutwa kazi
- Pigwa kalamu, kuonyeshwa mlango, kuonyeshwa paa, kumwaga unga-kufukuzwa kazini.
- Pigwa kitutu – pigwa na watu wengi
T
- Temea mate, kuonyesha mgongo, kuvalia miwani, kufumbia macho – kupuuza.
Mifano zaidi itaongezewa baadaye