Tanakali ni nini?
Hii ni tamadhali ya usemi ambayo hutumiwa kurejelea sauti inayoigiza jinsi kitu fulani kinavyotendeka. Tazama mifano ifuatayo:-
Tanbihi:
- Usitenganishe sauti ya tanakali kwa mfano: lia kwi kwi kwi – inafaa lia kwikwikwi
- Aidha usiweke alama ya mshangao mwishoni pa mlio. Kwa mfano: Lia kwikwikwi! Haya ni makosa inafaa lia kwikwikwi.
A
- Anguka kwa kitu chepesi kama vile penseli kacha.
- Anguka kwa mtu mnene bwata.
- Anguka kwa shilingi (chuma) sakafuni tangi
- Anguka majini chubwi.
- Anguka matopeni pwa.
- Anguka mchangani tifu.
- Anguka pahali pagumu pu.
B
- Bingirika bingiribingiri.
- Bwakia bwakubwaku
- Bweka bwebwebwe.
C
- Chapua miguu chapuchapu.
- Cheka kwakwakwa.
- Choka tiki.
- Churuzika churururu.
D
- Dondoka ndondondo.
- Dunda dududu.
E
- -eupe pepepe.
- -eusi pi/titititi.
F
- Funga ndindindi.
- Funika gubigubi.
- Furaha riboribo/furifuri/mpwitompwito.
G
- Giza totoro.
- Gugumiza gugugu
H
- Huzuni mpwitompwito.
J
- Jaa pomoni.
- Jaa sisisi.
K
- Kataa katakata.
- Komea komekome
- Kumbatiana papatu papatu.
- Kutopata ng’o
L
- Lala fofofo.
- Lewa ndi/chopi/chakari.
- Lia kwikwikwi.
- Lowa rovurovu/lovulovu/chepechepe.
M
- Maliza fyu.
- Matatizo tipitipi.
- Mchuzi rojorojo.
- Mulika mwaa.
- Mwagika mwa.
N
- Nuka fee/mff mff.
- Nukia hhh
- Nukia nhh.
- Nyamaza jii.
- Nyoka twaa.
P
- Pamba kochokocho.
- Ponea chupuchupu.
- Pukutika kupukupu.
R
- Regea regerege.
- Rowa rovurovu
S
- Saga tikitiki.
T
- Tafuna tafutafu.
- Teketea teketeke.
- Teleza parrr.
- Tiririka tiriri.
- Tokwa na jasho jekejeke.
- Tulia tuli.
V
- Vuma vuum.
- Vunjika kenyekenye.(kuvunjika kabisa)
- Vurugika vuruguvurugu.
Z
- Zimia zii.