Tashbihi ni nini?
Huu ni usemi wa kufananisha vitu viwili au zaidi ili kuleta msisitizo unaodhamiriwa na mzungumzaji au mwandishi. Mwanafunzi akitawala msamiati huu, huweza kujipatia alama nzuri katika uandishi wa insha kwa sababu msamiati wake upanda kiwango kingine. Tazama mifano ifuatayo:-
A
- Adimika kama wali wa daku; barafu ya kukaanga; kaburi la baniani; kivuli cha nzi; maziwa ya kuku.
- Amrisha kama mwanajeshi.
- Angalia huku na huko kama luja.
- Angua kicheko kama radi, jitu, fisi.
B
- Bahati kama mtende; mwana aliyezaliwa Ijumaa.
- Bahatika kama mwana aliyezaliwa Ijumaa.
- Baidika kama ardhi na mbingu.
- Banana kama ndizi.
- Baridi kama barafu.
- Batika kama mtende.
- Bidii kama mchwa.
- Bughudhi kama mwana wa kambo.
C
- Chafu kama fungo.
- Cheka kama mwehu.
- Chukiana kama wakewenza.
- Chungu kama shubiri, subiri.
D
- Dahadari kama mja anayekata roho.
- Dahadari kama nyoka anayekata roho.
E
- Ekundu kama damu.
- Embamba kama ufito/uzi
- Enda mbio kama umeme.
- Enea kama moto nyikani.
- Enea kama moto nyikani.
- Enye nguvu kama ndovu.
- Epesi kama paa.
- Epesi kama sufi/bua/joya.
- -epesi kama unyoya.
- Eupe pepepe kama bafta/pamba/theluji.
- Eusi tititi kama mpingo/lami/makaa/kaniki.
F
- Fahari kama kasri ya mfalme.
- Fanana kama shilingi kwa ya pili.
- Fuatana kama kumbikumbi.
- Fuatana kama magurudumu.
- Fupi kama nyundo/kidurango/kibikizi
- Furahi kama mama aliyepata mtoto salama salimini; tasa aliyepata mtoto; kibogoyo aliyeota jino; kipofu aliyetanabahi kuona.
- Fyatuka kama risasi.
G
- Ganda kama kigaga.
H
- Hakika kama mauti.
- Hasira kama za mkizi.
- Huzuni kama mfiwa.
I
- Imara kama chuma cha pua.
J
- Jahara kama pengo.
- Janja kama kifauongo, sungura.
- Julikana kama pesa.
K
- Kaidi kama punda/kirongwe.
- Kali kama Pilipili.
- Kali kama simba.
- Kali kama wembe.
- Kigeugeu kama kinyonga/lumbwi.
- Konda kama ng’onda.
- Kubwa kama uwanja wa ahera, bahari.
- Kuiga kama kasuku.
- Kupenda kama moyo wa mtu.
- Kutapatapa kama samaki atolewapo majini.
- Kutunza kama jicho la mtu.
- Kuwa na miguu mirefu kama korongo.
- Kuwa wa mwisho kama koti.
- Kuzurura kama mbwakoko.
- Kwenda pole kama kobe, konokono.
L
- Lafi kama fisi.
- Laini kama pamba.
- Lazima kama ibada.
- Lewa kama komba.
- Lia kama aliyeachwa na aila yote.
M
- Majuto kama ya firauni.
- Maneno mengi kama chiriku, kamusi.
- Maringo kama tausi.
- Mchafu kama fugo.
- Metameta kama nyota.
- Mfupi kama mbilikimo.
- Mjanja kama sungura, Abunuasi.
- Mjinga kama samaki.
- Mkali kama simbabuka.
- Mlafi kama fisi.
- Mnafiki kama panya, nduma kuwili.
- Mnyamavu kama kaburi/mava.
- Mrefu kama unju.
- Mrembo kama malaika.
- Msahaulifu kama nyati.
- Msiri kama kaburi.
- Mvumilivu kama mtumwa.
- Mwaminifu kama njiwa.
- Mwenye bidii kama mchwa, nyuki.
- Mwenye maneno mengi kama chiriku.
- Mwenye nguvu kama tembo/ndovu, kifaru.
- Mwenye uzembe kama kupe, chaza, kozi.
- Mwoga kama kunguru.
N
- Nata kama gundi.
- Nata kama gundi.
- Nene kama kiboko.
- -ngi kama njugu, mchanga ufuoni mwa bahari, siafu.
- Nuka kama kidonda, beberu, mzoga.
- Nuka kama kidonda.
- Nukia kama ruhani.
- Nyoka twa kama mwanzi.
P
- Paa kama moshi.
- Pana kama uwanja wa ahera.
- Pendana kama chanda na pete.
- Piga mbio kama aliyeona mizuka.
- Poa kama maji mtungini.
- Pofu kama jongoo.
- -pole kama kondoo.
- Pua kama kitara.
R
- Refu kama komanzi.
- Rembeshwa kama bibi arusi.
- Rembo kama hurulaini wa peponi.
- Ringa kama tausi.
- Roho ngumu kama paka.
S
- Safi kama mfua uji.
- Sauti nyororo kama ninga.
- Sauti nzuri kama kinanda, ndege, malaika.
- Sema kwa sauti kama radi.
- Sepetuka kama mlevi.
- Shingo nene kama mbuyu.
- Shirikiana kama kiko na digali.
- Shirikiana kama uta na upote.
- Shtuka kama aliyeona zamadamu.
- Sufufu kama mchanga.
T
- Tamu kama asali.
- Tamu kama halua.
- Tanda kama wingu la mvua.
- Tega masikio kama kelbu.
- Tema kama masuo.
- Tengana kama ardhi na mbingu.
- Tetea kama wakili.
- Tetemeka kama kondoo mwenye sufi haba.
- Tetemeka kama unyasi unaopigwa na upepo wa nyikani.
- Tia katikati kama mchuzi wa ugai.
- Tiririka kama maziwa ya ngamia.
- Tisha kama shetani.
- Tulia kama maji mtungini.
- Tumainia kama tai.
- Tumbo kubwa kama kiriba.
- Tunzana kama kisu na uo.
U
- Uso kama kifuu.
V
- Vutia kama zuhura.
W
- Washa kama upupu.
- Wasiwasi kama kuku mgeni, mwasi.
- Wazi kama mchana.
- Weupe wa theluji – sio wa mtu.
- Weusi kama wa mpingo, kizimwili.
- Wima kama msonobari.
- Wivu kama joka la mdimu.
Z
- Zito kama nanga.
- Zito kama nanga.
- Zurura kama jibwa liso kwao.
Tanbihi: Mwanafunzi au mlumbi awaye yule anaweza kufananisha kwa kutumia maneno kama vile:
- kama
- mithili ya
- sawasawa na
- ungedhani