Tashdidi ni fani ya lugha inayotumia maneno mawili yaliyo na maana moja kuleta msisitizo katika uandishi. Hizi ni kati ya tashdidi ambazo zimekusanywa kwa ustadi sitazokusaidia kupamba Insha yako vilivyo. Tazama mifano ifuatayo:-
- Adabu na nidhamu
- Akili na maarifa
- Alifoka na kung’aka
- Bidii na juhudi
- Bora na mufti
- Duwaa na kubung’aa
- Eleza na kufafanua
- Fika na kuwasili
- Fikiri na kutafakari
- Gundua na kufahamu
- Hamu na hamumu
- Haribu na kuvuruga
- Hasira na ghadhabu
- Heshimu na stahi
- Hiriki na kuangamiza
- Hofu na wahaka
- Imba na kughani
- Jaa na kufurika
- Jidai na kujinata
- Julisha na kufahamisha
- Kaa na kubarizi
- Kamsa na mayowe
- Karipia na kukemea
- Kelele na mayowe
- Kerwa na kereketwa
- Keti na kukaa
- Kubaliana na kuafikiana
- Kuchanganua na kupambanua
- Kufa na kufariki
- Kujisafisha na kujinadhifisha
- Kula na kushiba
- Kumbuka na kudhukuru
- Kumbuka na kutambua
- Kunionya na kunikanya
- Kuomba na kusihi
- Kuona na kuangalia
- Kupamba na kuremba
- Kwa dharau na bezo
- Lala na kusinzia
- Latifu na mpole
- Machugachuga na wasiwasi
- Majonzi na simanzi
- Maringo na madaha
- Mrembo na mlimbwende
- Mtiifu na mwadilifu
- Ng’aa na meremeta
- Nia na azma
- Nyamaza na kunyamaa
- Onya na kukanya
- Penya na kupenyeza
- Pigwa na kuchabangwa
- Polepole na taratibu
- Pongeza na kuongera
- Pongeza na kushukuru
- Safi na nadhifu
- Sema na kunena
- Sema na kukuli
- Shangaa na kubung’aa
- Shangaa na kusangaa
- Shikwa na kukamatwa
- Sikia na kusikiliza
- Subiri na kungojea
- Taabu na dhiki
- Tabasamu na kucheka
- Tafakari na kuvuta taswira
- Tambua na kung’amua
- Tamka na kusema
- Tembea na kuzurura
- Tiririka na kumwagika
- Toka na kutoweka
- Tosheka na kukinai
- Tua na kutulia
- Tuliza na kuliwaza
- Tunza na kuhifadhi
- Uliza na kusaili
- Uzuri na urembo
- Vaa na kuvalia
- Vishindo na vituko
- Vuta na kuburura
- Wasiwasi na shaka
- Wasiwasi na wahaka