Haya ni maneno yaliyo na maana moja na huumika katika jozi ili kuleta msisistizo katika uzungumzaji au uandishi. Sana sana huwa vitenzi. Tazama mifano ifuatayo:
1. Ardhi na mbingu – tofautiana
2. Asili na jadi -zamani sana.
3. Balaa na belua – matatizo makubwa.
4. Bure bilashi – bila sababu yoyote ile.
5. Daima dawamu – bila kukoma; kila wakati.
6. Doto na Kurwa – pacha
7. Enzi na dahari -tangu zamani.
8. Farka na mitafaruki – kutokubaliana / kutosikilizana
9. Ficha na kufichua – sitiri na kuonyesha
10. Haambiliki hasemezeki – hasikii analoambiwa
11. Hajailalia hajaiamkia -hajaitarajia, jambo ambalo hulitarajii kamwe.
12. Hajijui hajitambui -kuchanganyikiwa k.m. kutokana na uuele, umaskini, ulevi n.k.
13. Hakanywi hakanyiki -Utukutu uliopita kiasi
14. Hakiri habali -hakubali jambo.
15. Hali na mali – kwa kila hali.
16. Haliki hatafuniki -utundu uliopita kiasi.
17. Hana bee wala tee -maskini kupindukia.
18. Hana hanani Sina sinani -umaskini wa kupindukia.
19. Hana hatia wala taksiri – hana hatia yoyote.
20. Hana kazi wala bazi -hana kazi yoyote ile.
21. Hana ngoma wala maulidi -kutokuwa na furaha.
22. Haoni hasikii -kupumbazwa au kulipenda. jambo kupita kiasi.
23. Hapiki hapakui -mzembe mno.
24. Hayanihusu damu wala usaha -hayanihusu kwa kila hali.
25. Hayanihusu ndewe wala sikio – kutokuwa na haja na mambo fulani.
26. Hazidishi hapunguzi -hayana athari yoyote
27. Heri na shari – uzuri na ubaya
28. Inda na tadi – kuwa na uchoyo na ujeuri
29. Jembe na mpini – kushikamana kutenda kazi
30. Juha na majinuni -mjinga sana
31. Juu chini -kwa bidii sana.
32. Kiguu na njia -kutembea sana.
33. Kondoo na mbwa – maadui
34. Kuanzia shina hadi kilele -kila sehemu kila jambo.
35. Kufa kuzikana – kupendana sana
36. Kufa na kupona – hali yoyote ile
37. Kujitahidi kufa kupona – kujitahidi sana.
38. Kutia na kutoa -kufikiria sana.
39. Kutojali togo wala jando -kutojali kwa vyovyote vile.
40. Kutwa kucha -mchana na usiku, kila wakati
41. Kuwaza na kuwazua -kufikiria sana.
42. Kwa heri na kwa shari -kwa uzuri na kwa ubaya.
43. Kwa la jua na mvua – kwa hali zote
44. Kwa mapana na marefu -kwa kila njia.
45. Mabonde na milima -safari ndefu.
46. Maji na mafuta – kutoelewana
47. Miaka nenda miaka rudi – miaka mingi.
48. Misitu na nyika -safari ndefu.
49. Mito na maziwa -safari ndefu.
50. Mshale na podo – kufaana na kutunzana.
51. Nipe nikupe -kuwa na masharti.
52. Pua na mdomo – karibu sana.
53. Rafiki wa kufa kuzikana – rafiki mkuu.
54. Sahani na kawa – kuwa pamoja au kupatana
55. Sakafu na dari – kutazamana tu
56. Salama salimini -bila hatari yoyote ile.
57. Shangwe na hoihoi – furaha
58. Shibe na njaa – furaha na huzuni
59. Si hayati si mamati -kuugua sana.
60. Simanzi na majonzi – huzuni kubwa.
61. Suna na faradhi – hiari na lazima.
62. Udi na uvumba – kwa kila hali
63. Ugonjwa usiosikia dawa wala kafara – ugonjwa usiotibika.
64. Upende usipende – lazima.
65. Uso kwa kioo – kutazamana vizuri
66. Uvumba na ubani / Udi na ambari -kwa bidii sana.
67. Zogo na zahama – fujo na ghasia nyingi.