Sentensi huwa na sehemu kadhaa madhalani nomino, kivumishi, kitenzi, kiunganishi, kihusishi, kielezi, kiwakilishi na kihisishi.
Ipo mipangilio kadhaa laini nitashughulikia michache.
Nomino + kivumishi + kitenzi + kielezi
Km. Mwanasheria huyu ametoka Amerika.
Nomino + kitenzi + kielezi
Km. Bibiarusi anatembea kwa madaha.
Kiwakilishi + kitenzi + kielezi
Km. Huyu anaimba vizuri.
Kitenzi + Kielezi.
Km. Wanaruka Kimaasai.
Nomino + kitenzi + kihusishi + nomino + kitenzi
Km. Mwalimu aliyesimama kando ya darasa ameenda.
Kiwakilishi + kitenzi kisaidizi + nomino + kimilikishi
Km. Wao ni wana wetu.
Nomino + kitenzi + kihusishi + nomino
Km. Gatanga amesimama mkabala na darasa.
Nomino + kivumishi kiashiria + kitenzi kisaidizi + kimilikishi + kiwakilishi + kivumishi kiashiria + kitenzi kisaidizi + kimilikishi.
Km. Mtoto huyu ni wangu, yule pale ni wake.
Kitenzi
Km. Alinichapa.
Ipo miundo zaidi na vievile inayotatanisha zaidi, lakini utaishughulikia kwa kina ufikapo shule ya upili. Kwa sasa miundo niliyoirorodhesha inatosha kukuwezesha kujibu maswali ya K.C.P.E.
Fanya maswali yaliopo hapa chini ili kujitadhimini.
Zoezi
[ays_quiz id=”1″]