Skip to content

Kiswahili Mujarabu

Atangaye na jua hujua

  • Nyumbani
  • Yaliyomo
    • Sarufi
    • Kuandika
      • Utahini wa Insha KCPE
      • Insha Mbalimbali
      • Aina za insha
    • Kusikiliza na kuongea
    • Msamiati
    • Kusoma
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Toggle search form

Ufundishaji wa ufahamu

Posted on By Harun Mbijiwe 6 Comments on Ufundishaji wa ufahamu

Ufahamu ni kifungu ambacho hufundishwa na kutahiniwa katika shule za msingi. Jambo linalotahiniwa katika ufahamu ni kuekewa kwa mwanafunzi. Ili mwanafunzi aelewe yapo mambo kadhaa anahitaji kuyaelewa.

  1. Kwa kawaida haya ya kwanza hutanguliza mada kuu ya kifungu.
  2. Kila kifungu huwa na maudhui yanayolengwa kutoka mwanzo hadi mwisho.
  3. Kila aya hundwa ikilenga maudhui ya kifungu kizima. Kila aya huzungumzia hoja moja inayolenga mada kuu ya kifungu.
  4. Kila sentensi hujaliza maudhui ya aya husika ikilenga hoja katika aya hiyo.
  5. Aya ya mwisho huleta hitimisho la kifungu kizima kwa kuleta wazo la wasia, kuhimiza au kutia shime na kutoa malengo ya kifungu ili kuunga yaliyozungumziwa awali.
  6. Maswali hutahiniwa yakilenga aya kwa aya hata kama yataulizia msamiati fulani mwanafunzi atumie muktadha ili kupata maana.

Ili kukielewa kifungu na kuweza kujibu maswali aliyoulizwa mtahiniwa anahitaji kufanya nini?

1. Asome kwa kina akikagua maudhui ya kila aya. Apate mambo muhimu yanayotajwa ili kuyaelewa maudhui au wazo kuu katika kila aya. Aandike pembeni yanayojitokeza kwa mukhtasari.

2. Ayasome maswali pamoja na majibu yake, halafu arejelee ufahamu kuona kubwa jibu linajitokeza hadharani au kwa undani katika kifungu.

3. Atoe majibu mawili yaliyo mbali na ukweli wa ufahamu. Atumie uwezo wa usanisi ili kuweza kuteua jibu sahihi kati ya mawili yaliyobaki.

4. Akiishapata jibu arejelee swali tena ili aone kama ameteua jibu sahihi.

Tanbihi:

Mwanafunzi asijaribu kujibu maswali kwa kutumia akili au mawazo yake hata kama swali ni rahisi vipi. Kila wakati arejelee ufahamu ili kupata ukweli wa mambo.

 

 

Post Views: 166
Kusoma, Mawaidha ya Ufundishaji

Post navigation

Previous Post: Uchanguzi wa Sentensi
Next Post: Methali Zinazolandana

Machapisho mapya

  • Barua
  • Insha ya Methali
  • Tashbihi
  • Ngeli na maelezo yake
  • Hotuba

Kumbukumbu

  • June 2025
  • January 2025
  • May 2024
  • February 2024
  • January 2024
  • September 2023
  • July 2023
  • April 2023
  • March 2023
  • September 2021
  • August 2021
  • July 2021
  • June 2021

Kategoria

  • Aina za insha
  • Insha Mbalimbali
  • Kusikiliza na kuongea
  • Kusoma
  • Majibu
  • Mawaidha ya Ufundishaji
  • Msamiati
  • Sarufi
  • Utahini wa Insha KCPE

Copyright © 2025 Kiswahili Mujarabu.

Powered by PressBook Green WordPress theme